LEWIS HAMILTON ASHINDA MBIO ZA CHINESE GRAND PRIX

Dereva wa Mercedes, Lewis Hamilton, ametawala mbio za langalanga za Chinese Grand Prix na kupata ushindi wake wa kwanza mwaka huu.

Hamilton amepata ushindi katika mbio hizo zilizofanyika huku barabara zikiwa na maji maji ya mvua na kuchuana vikali na mpinzani wake Sebastian Vettel wa Ferrari.

Katika mbio hizo Vettel amemaliza katika nafasi ya pili na kuashiria mwaka huu ushindani wa ubingwa utakuwa ni baina ya madereva hao wawili.

Dereva wa Red Bull, Max Verstappen, alisogea kutoka nafasi ya 16 na kumaliza watatu katika mbio hizo.
             Muingereza Lewis Hamilton akishangilia kwa kurusha juu kikombe cha ushindi
             Lewis Hamilton akichagiza sherehe za ushindi wake kwa kumwaga champagne
 Lewis Hamilton (katikati) akiwa na Sebastian Vettel wa kwanza kushoto na Max Verstappen (kulia)
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post