LIGI KUU TANZANIA BARA: MECHI 6 KUPIGWA WIKENDI HII

Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea wikendi hii, huku Simba na Azam FC zikisubiri hadi Jumatatu kusaka point tatu katika viwanja viwili tofauti vya ugenini.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, Jumamosi Aprili 8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea itaialika African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mechi nyingine kwa siku ya Jumamosi Aprili 8, mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera wakati wakati siku ya Jumapili Aprili 09, mwaka huu Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Ligi inatarajiwa kuendelea Jumatatu Aprili 10, mwaka huu kwa michezo miwili ambako Simba itakuwa mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa Sugar itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post