LIONEL MESSI AFUNGA GOLI LAKE LA 500 BARCA IKIIFUNGA REAL MADRID

Lionel Messi amefunga goli lake la 500 akiwa na Barcelona katika dakika za majeruhi na kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Real Madrid iliyobakia na wachezaji kumi katika dimba la Bernabeu.

Kwa ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi sawa na Real Madrid katika ligi ya La Liga wakiongoza, lakini Madrid wao wanamchezo mmoja mkononi.

Katika mchezo huo Casemiro alikuwa wa kwanza kuwafungia wenyeji goli kabla ya Messi kusawazisha na Ivan Rakitic kuifungia goli la pili Barcelona na kisha Sergio Ramos alionyeshwa kadi nyekundu.

Mchezaji aliyetokea benchi James Rodriguez aliifungia Real Madrid goli la kusawazisha lakini Lionel Messi akafunga goli la tatu katika dakika ya 101.
                                                 Casemiro akifunga goli la kwanza katika mchezo huo 

                                     Lionel Messi akifunga goli la tatu lililoipa ushindi Barcelona
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post