LIVERPOOL KUWAKOSA NYOTA WAKE WATATU KATIKA DABI YA LEO

LIVEROOOL itawakosa nyota wake watatu wa nguvu,nahodha Jordan Henderson,Adam Lallana na Daniel Sturridge kwenye mchezo wake wa leo Jumamosi wa ligi kuu nchini England dhidi ya Everton unaotambulika kama dabi ya Merseyside kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Akifanya mahojiano na mtandao wa ESPN,kocha mkuu wa klabu hiyo,Mjerumani Jurgen Klopp amekiri kuwa na wakati mgumu katika upangaji wa kikosi chake kuelekea mchezo huo ambao ni wa 228 kwa miamba hiyo kukutana na Everton.


Akimwelezea Lallana,Klopp  amesema nyota huyo atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha mwezi mmoja akiuguza jeraha la nyama za paja alilolipata hivi karibuni wakati akiichezea England kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ujerumani.

Henderson ambaye amekosa michezo minne iliyopita ya Liverpool bado anasumbuliwa na msumivu ya mguu.Klopp amesema Henderson alijaribu kurejea lakini akajitonesha jeraha hilo.

Kwa upande wa Sturridge,Klopp amesema mchezaji huyo hana nafasi ya kucheza mchezo wa leo kwani ndiyo kwanza amerejea mazoezini hivi karibuni akitokea kwenye majeruhi yaliyomweka nje ya uwanja tangu mwezi Februari.

Wakati huohuo Klopp amesema nyota wake wawili Philippe Coutinho na Roberto Firmino wamerejea salama kikosini wakitokea nchini kwao Brazil walikokuwa wamekwenda kuichezea timu yao ya taifa na kuipa tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia litakalofanyika mwakani nchini Urusi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post