LIVERPOOL YAZIDI KUPAMBANA KUBAKIA NAFASI NNE ZA JUU

Liverpool imeongeza nafasi ya kujihakikisha kumaliza katika nafasi za juu nne za msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Everton kwa magoli 3-1.

Sadio Mane aliipatia Liverpool goli la kuongoza baada ya kugongeana vyema na Roberto Firmino na kuachia shuti lililokwenda kujaa kwenye kona ya goli.

Matthew Pennington aliifungia Everton goli la kusawazisha likiwa ni goli lake la kwanza akiwa na Everton akicheza kwa mara ya kwanza katika msimu huu.

Coutinho aliwatoka wachezaji wa Everton na kufunga kwa shuti la kuzungusha na kisha baadaye akamtengenezea Divock Origi aliyetokea benchi na kufunga goli la tatu.
                           Sadio Mane akiachia shuti na kufunga goli la kwanza la Liverpool 
               Countinho akipiga shuti la mpira wa kuzungusha na kufunga goli la pili 
                            Sadio Mane akichezewa rafu na Tom Davies ambaye alipewa kadi 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post