LUKUVI ATOA SIKU SABA KWA WA BUNGE KULIPA MAMILIONI

Na Florian Kilimila

Mwanza. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameendelea kugeuka kaa la moto kwa wanaokiuka sheria na taratibu za ardhi mkoani Mwanza baada ya kutoa siku saba hadi Mei 5, kwa Mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor kulipa deni la Sh529 milioni analodaiwa kwenye eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 39 lililopo Kata ya Buhongwa jijini Mwanza.

Alitoa agizo baada ya kubaini deni hilo katika baadhi ya mafaili kutoka idara ya ardhi jiji la Mwanza aliyoyapitia wakati wa ziara yake inayoendelea jijini hapa, Lukuvi ameonya kuwa iwapo hatalipia hadi muda huo, Serikali italitwaa eneo hilo na kulipangia kazi nyingine ikiwamo kuwagawia wananchi.

Huku akiwakazia macho maofisa ardhi wa jiji, Lukuvi alihoji sababu za idara hiyo kuwabana wananchi wa kawaida na kuwafumbia macho viongozi wa Serikali na kisiasa wanaodaiwa kodi na ushuru wa ardhi.

Akizungumza kwa simu kuhusu deni hilo Mansoor alisema suala la ulipaji wa kodi ya eneo hilo liko mahakamani tangu mwaka jana ingawa upande wa pili ambao ni halmashauri haujitokezi kwenda kusikiliza.

Alisema eneo hilo limezungukwa na mlima uliojaa mawe makubwa na kwamba ni ekari tano pekee ambazo anatakiwa kuzilipia kodi.

“Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia halmashauri ya jiji ili kubadilishiwa hati kwa kuwa eneo linalofaa kuendelezwa ni ekari tano pekee, zilizobaki ni milima ambayo haipaswi kuiendeleza isipokuwa kuchimba mawe kwa ajili ya ujenzi au kuponda kokoto,” alisema Mansoor
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post