MAAGIZO MANNE YA TFF KUHUSU MGOGORO WA KLABU YA LIPULI FC

Kwa muda mrefu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefuatilia kwa kina mgogoro wa kiuongozi ndani ya klabu ya Lipuli FC ya Iringa.
Baada ya uchunguzi wake, TFF imetoa maagizo manne yafanyike mara moja.
1.Klabu ya Lipuli ifanye uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wake.
2.Kamati ya uchaguzi ya TFF itasimamia mchakato mzima wa uchaguzi huu.
3.Uchaguzi huu utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Lipuli FC uliofanyika tarehe 22 Juni 2014.
4.Kamati ya uchaguzi ya TFF itahakiki na kutoa orodha ya wapiga kura.
MKUTANO MKUU WA TFF
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kimekutana leo Jumapili Aprili 9, 2017 na miongoni mwa maamuzi yake kikao kimeamua kuwa Mkutano Mkuu wa TFF, utafanyika Jumapili ya Agosti 12, 2017.
Miongioni mwa ajenda katika mkutano huo, itakuwa ni uchaguzi mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi huo utachagua Rais wa TFF, Makamu Rais wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post