MAAGIZO YA WAZIRI NCHEMBA KUHUSU KUTOWEKA KWA MSANII ROMA NA WENZAKE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa ameshtushwa na kutoonekana kwa mwanamuziki Roma Mkatoliki pamoja na wenzake waliokamatwa wakiwa katika Studio za Tongwe Records.
Akiwa kama Waziri mwenye dhamana ameagiza Jeshi la Polisi kufuatilia kujua undani wa tukio hili, hatma ya wasanii hao na pia watoe taarifa kwa umma kuhusu mwenendo wa tukio leo.
Waziri nchemba aliyasema hayo jana kupitia ukurasa wake w a Instagram ambapo aliandika, Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa ,zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma.”

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post