MAAJABU: MWANAMKE MWENYE SEHEMU MBILI ZA UKE APATA UJAUZITO

Mwanadada Krista Schwab mwenye umri wa miaka 32 ameenda kinyume na utabiri wa madaktari waliomwambia hana uwezo wa kuzaa kwa sababu ya kuwa na sehemu mbili za uke.
Mwanamke huyo aliyezaliwa akiwa na sehemu mbili za uke, sehemu mbili za mifuko ya uzazi pamoja na matumbo mawili ya uzazi sasa anatarajia kupata mtoto wa kiume baada ya muda mrefu wa kuhangaika pamoja na mumewe kutafuta mtoto.
Krista anayeishi Washington huko Marekani aligundulika kuwa na hali hiyo ya kipekee inayojulikana kitaalamu kama ‘uterus didelphys’ alipokuwa na umri wa miaka 12.
Mwanamke huyo alitambua kuwa ana mifuko miwili ya uzazi alipokuwa na umri wa miaka 12 lakini hakutambua kama ana sehemu mbili za uke mpaka alipofikia umri wa miaka 30.
Madaktari walimwambia kuwa hawezi kupata ujauzito kutokana na hali yake. Alihangaika sana na aliwahi kubeba mimba mara mbili ambazo ziliharibika jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kukosa matumaini ya kupata mtoto.
Krista sasa ana ujauzito wa miezi mitano na yeye na Mume wake sasa wanatarajia kupata mtoto wa kiume.
“Kwa muda wa miaka mingi mimi na mume wangu tumekuwa tukilia, tukiomba na kuwa na ndoto za kupata mtoto. Tumemtafuta kwa hali na mali kwani tulitaka mtoto kwa hali na mali.” Alisema Krista.
Baada ya miaka mingi ya kuwa na ndoto ya kupata mtoto wa miujiza, Krista alinunua kipimo cha ujauzito pasipokuwa na matumaini yoyote.
“Baada ya kupima ujauzito kwa mara zaidi ya 1000 nilikata tamaa kabisa ya kupata ujauzito. Mwezi wa disemba niliamua kujaribu tena na nilinunua kipimo cha bei ghali, ambacho mimi na mume wangu tulidhani ni upotevu tu wa pesa” Alisema
Alisema kuwa amekuwa akiomba na kujipa matumaini huku akisubiri, lakini baada ya muda mrefu alikata tamaa kabisa, lakini kipimo kiliwashtua wote kwa kuleta matokeo ambayo hawakuwa wanayatarajia.
“Nilipoona kipimo kimetoa matokeo chanya, nilianguka chini kwa kilio. Tulishtuka na kufurahi  sana, hasa mume wangu” Alisema Krista
Aliongeza kuwa tokea alipokutana na mume wake alimwambia kuwa hana uwezo wa kupata ujauzito hivyo mara zote walipofanya mapenzi hawakutumia kinga.
Tatizo hilo la ‘uterus didelphys’ huusishwa mioja kwa moja na kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito. Lakini kwa Krista imekuwa muujiza kwani mtoto yupo katika mfukoo wa uzazi ambao hauwezi kutoa mbegu za uzazi.
Alisema kuwa mayai pekee ya uzazi yaliyokuwa yakifanya kazi ni yale yaliyo katika mfuko wa uzazi wa kulia. Na kutokana na kuwapo kwa uwazi kidogo sana kati ya mifuko hiyo miwili ya uzazi, ni vigumu kwa yai kutoka mfuko wa kulia kwenda mfuko wa kushoto.
“Ni ajabu sana kwa kuwa madaktari bado hawaelewi. Ukweli wa kuwa mjamzito katika tumbo la kushoto ambalo ni vigumu kwa mbegu za uzazi kufika humo. Ingawa ninaifurahia ndoa yangu siku zote” Alisema Krista aliyeonekana kuwa na furaha iliyochangiwa na hali ya yeye kuwa mjamzito.
 She wants her pregnancy to give hope to other sufferers who are desperate to conceive
Krista na Mumewe wakifurahia na kumngoja kwa hamu mtoto atakayezaliwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post