MAAJABU : MWANAMKE WA MIAKA 23 AMBAKA DEREVA TAX WA KIUME NCHINI MAREKANI

Mwanamke mmoja katika jimbo la Ohio nchini Marekani ameshtakiwa kwa kumbaka dereva mmoja wa teksi kwa kutumia kisu kabla ya yeye na mwanamume mwengine kumuibia kulingana na maafisa wa polisi.

Brittany Carter mwenye umri wa miaka 23, anadaiwa kufanya tendo la ngono na dereva huyo mwenye umri wa miaka 29 huku Corey Jackson mwenye umri wa miaka 20 akimshikia kisu shingoni.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wawili hao waliiba dola 32 kutoka kwa mwathiriwa kabla ya kutoroka katika eneo la mkasa katika mji wa Findlay.
Hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,luteni wa polisi Robert Ting alisema. Pengine ilikuwa hali ya kumpumbaza kwa sababu pia walimuibia pesa.
Unyanyasaji huo ulitokea baada ya bi Carter kumuita dereva wa teksi hiyo ya kampuni ya Trinity Express Cab mapema mnamo tarehe 28 mwezi Januari, kulingana na maafisa wa polisi.
Bi Carter anakabiliwa na shtaka la ubakaji pamoja na lile la uhalifu katika mahakama ya kaunti ya Hancock.
Alishtakiwa mara mbili kwa makosa ya dawa za kulevya mwaka 2016 na anadaiwa kumiliki dawa ya kulevya aina ya heroine.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post