MADHARA YA KAFEINI (CAFFEINE) NDANI YA MWILI WA BINADAMU

Watu wengi huianza siku yao kwa kunywa vinywaji mbalimbali kama chai, soda juisi au maji. Unapovitumia vinywaji hivi mara nyingi huwazi kama vina madhara katika afya.
Vinywaji kama vile soda, kahawa, chai na vile vya kuongeza nguvu huwa vina aina ya Kafeini (Caffeine) ambayo huwa na madhara mengi mwilini pale vinapotumika kwa wingi.
Kwa upande mmoja vinywaji hivi huwa na faida. Utafiti umeonyesha kuwa huchangamsha, kukupa nguvu na kuiweka akili katika hali ya utulivu hasa unapoianza siku.
Vilevile vinywaji hivi kama vile kahawa huwa na madhara pale ambapo vinapotumika kwa muda mrefu na kwa mazoea.
Haya hapa ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na Kafeini
Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Kafeini  huongeza kiwango cha asidi katika tumbo na hupunguza kiwango cha maji mwilini.
Mfumo wa damu na hewa
Kafeini inapoingia katika damu huchukua muda wa saa moja mpaka mbili kufikia maeneo mbalimbali ya mwili, hii itasababisha msukumo wa damu kuongezeka ndani ya muda mfupi. Kwa hivyo kiwango kikubwa cha Kafeini katika mwili kinaweza kupandisha kasi ya mapigo ya moyo na kusababisha matatizo katika mfumo wa hewa.
Mfumo wa uzazi
Kafeini husafiri katika damu na kuifikia ‘placenta’, hivyo kwa mama mjamzito, matumizi ya vinywaji vyenye Kafeini  huweza kuathiri mapigo ya moyo ya mtoto aliyeko tumboni. Vilevile Kafeini huweza kuharibu mimba na kuifanya itoke.
Huathiri mifupa na misuli ya mwili
Kafeini  inaweza kuvuruga mfumo wa kimetaboliki na ufyonzaji wa wa madini ya calcium ambayo huathiri mifupa na kusinyaa kwa misuli. Pia husababisha kupungua kwa uzito wa mifupa na hii huiweka mifupa ya mwili katika hatari ya kuvunjika kirahisi. Inatambulika kuwa Kafeini  husababisha kutolewa kwa madini ya calcium katika mifupa kupitia mfumo wa mkojo.
Mfumo wa figo
Kafeini  huzifanya figo kutoa maji mengi nje ya mwili. Hivyo matumizi ya muda mrefu ya vinywaji vyenye Kafeini  husababisha kemikali iitwayo ‘oxalates’ ambayo ikiungana na damu hutengeneza ‘calcium oxalates’ ambayo husababisha uwepo wa vijimawe vingi katika figo.
Watu wengi waliojizoesha kutumia kahawa na chai yamkini hawapendelei kusikia madhara ya Kafeini kiafya. ila kupitia ujumbe huu inabidi kupunguza matumizi ya vinywaji hivi mara kwa mara.
Kama umekuwa ukitumia vinywaji vyenye Kafeini kwa muda mrefu na ukaviacha kwa haraka, yawezekana ukapata kizunguzungu, maumivu ya kichwa, uchovu, muwasho na hata kukosa umakini katika kazi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post