MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI KATIKA MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kus...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.

Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.

'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi laki Tano.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

Aidha, Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo zile za Elimu na Afya.

Akijibu Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Moshi, Kilimanjaro.
30 Aprili, 2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI KATIKA MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI
MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI KATIKA MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI
https://1.bp.blogspot.com/-nOF4VVxL4Ww/WQW4kbtEyFI/AAAAAAAAaTQ/bPCqzJdBqYMNwdcLxIyM9JWNOa6jALu6ACLcB/s1600/tmp_26807-m10.JPG100701425.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-nOF4VVxL4Ww/WQW4kbtEyFI/AAAAAAAAaTQ/bPCqzJdBqYMNwdcLxIyM9JWNOa6jALu6ACLcB/s72-c/tmp_26807-m10.JPG100701425.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/magufuli-ahudhuria-ibada-ya-jumapili_30.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/magufuli-ahudhuria-ibada-ya-jumapili_30.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy