MAHAKAMA NCHINI KENYA YAZUIA UAMUZI WA RAIS DKT MAGUFULI

Mahakama ya Kazi na Ajira nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo baada ya madaktari watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.

Zuio hilo limekuja ikiwa ni siku chache tangu serikali ya Tanzania ilipokubali ombi la Kenya la kutuma madaktari 500 kwenda kufanyakazi nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari wa Kenya uliodumu kwa siku 100 na kuiacha sekta hiyo ya afya katika hali mbaya.

Madaktari hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.

Madaktari waliofungua Kesi nchini Kenya kupinga uamuzi huo ni Teddy Menza, Yunas Mohamed Shee, Lilian Nyambeki Magara, Victor Muia Mutisya na Aldran Falivian.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, Dkt. Mpoki Ulisubisya alisema kuwa zaidi ya madaktari 470 walituma maombi kutaka kwenda kufanyakazi nchini Kenya.

Kwa upande mwingine Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) pamoja na wadau wengine mbalimbali wameitaka serikali kutopelekea madaktari nchini Kenya hadi hapo serikali ya nchi hiyo itakapomaliza mgogoro na madaktari wake na wajiridhishe juu ya usalama wa watakaopelekwa Kenya.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post