MAHAKAMA YAKUBALI AGNES MASOGANGE AKAMATWE TENA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa Agnes Gerald Waya maarufu kama Agnes Masogange (28) baada ya kushindwa kwa mara ya pili kufika mahakamani wakati kesi yake ikipangwa kutajwa.
Upande wa Jamhuri ulimwambia Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana lakini mtuhumiwa, wadhamani na mawakili wote hawakufika mahakamani.
Hii ni mara ya pili mtuhumiwa huyo kutofika mahakamani kesi yake ikipangwa kutajwa na hali hiyo ilimlazimu wakili wa serikali, Adolf Nkini kuomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo.
Hakimu alikubali maombi ya wakili huyo kwa sababu ni kwa mara ya pili mtuhumiwa hajafika mahakamani tena bila hata kutoa taarifa yoyote.
Katika kesi ya msingi, Msogange anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam jambo ambalo ni kinyume na sheria ya dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Masogange anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Februari 7 hadi 14 mwaka huu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam. Baada ya kushtakiwa kwa kosa hilo, Masogange aliachiwa kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya TZS milioni 10 kila mmoja na mshatakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post