MAKALA : HUYU ULIMWENGU HAUMJUI, HEBU MPELEKENI DUNIANI.

SHARE:

Jumamosi ya tarehe 16 April 2017 Emma Morano ambaye Vitabu vya Dunia vimemtambua kuwa na Umri Mrefu zaidi alifariki dunia. Morano aliyeku...

Jumamosi ya tarehe 16 April 2017 Emma Morano ambaye Vitabu vya Dunia vimemtambua kuwa na Umri Mrefu zaidi alifariki dunia. Morano aliyekuwa Mkazi wa Mji wa Verbania Kaskazini mwa Italia alifariki dunia akiwa na Umri wa miaka 117.

Wakati dunia ikiwa imeaminishwa kuwa Emma Morano ndiye Mwanadamu mwenye Umri mkubwa zaidi aliyekuwa hai kwa mujibu wa Guineas Word of Record, lakini ukweli ni kuwa Dunia haina Taarifa sahihi.
Kwa taarifa zaidi za Moran ingia hapa: mobile.reuters.com/article/idUSKBN17H0JH

UKWELI HUU HAPA.
Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikiria Rekodi ya kula Chumvi nyingi Duniani kwa sasa.
Mzee Ambilikile Panja ambaye alishuhudia Vitaa kuu zote Mbili za Dunia kwa ukaribu, anakadiriwa kuwa na Umri wa wa zaidi ya miaka 127 leo.

Mkazi huyo wa Kitongoji cha Izyika ambaye kwa sasa haoni wala Kusikia vyema amemsimlia mwandishi wa makala hii kuwa wakati wa Vita ya Maji Maji dhidi Wakoloni alikuwa tayari anachunga mifugo ya Baba yake Marehem Mwanyaluke Panja.

Mzee Ambilikile Panja Kabila Mndali kutoka Tarafa ya  Bundali Ileje anasema, Wakati wa Vita ya Maji Maji "Wazazi wetu walitwambia tukiona Wazungu tuiache mifugo tukimbie kurudi nyumbani" anasema Mzee Panja.
Mzee Panja ambaye kwa sasa hawezi kusimama wala kutembea anasema, Vita ya Kalenga (Mkwawa) haikuwahi kufika kwao Ileje, Isipokuwa Vita ya Pili ya Dunia ilifika mpaka Mbozi.

Anasema Vita ya Hitler, (Vita ya Pili ya Dunia) ilianza Wakati yeye akiwa ameshakimbia kutoka Ileje na kuhamia Mbozi (Kijiji cha Ihanda) baada ya Kupora Mke wa Chifu.  Anasema yeye mwenyewe alishuhudia Mzungu aliyekuwa na Nywele mwili Mzima mithili ya Mnya akiwa amekimbia kujiokoa na Maadui zake. "Tulipo muona huyo Mzungu, tulidhani ni Mnyama kumbe ni Binadamu", anasema kwa Kindali huku akishusha Kicheko hafifu kilichofuatiwa na Kikohozi cha Ukongwe.

Mzee Ambilikile anasema Wakati wa Vita ya Hitler tulilazimika kuchimba Mashimo {Mahandaki} ya kujificha kuleee Lwibhaaa (Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ihanda) <<Handaki hili lipo mpaka sasa eneo hilo.>>
Mzee Panja ambaye mtoto wake wa Kwanza Marehemu Leonard Panja alifariki dunia kutokana na Uzee, mwaka 2014 akiwa na Umri wa miaka 98 anasema Marafiki zake wote, pamoja na Maadui zake wakiwamo Machifu aliokuwa anapingana nao, wote wameshatangulia mbele za haki amebaki pekee yake.
"Mimi nilitoka Kapelekeshi nikaenda kuishi Ibungu Itumba na baadae nikahamia hapa Mbozi. Hapa nilikuja na Mke wangu Mkubwa Agnes Mlawa na Watoto wangu watatu Leonard, Lassary na Pitros pamoja na Zacharia Panja na marehemu Mbonasi Panja (watoto wa ndugu zake)"
anasimulia mzee Panja.

Mzee Ambilikile kwa sasa ni Kikongwe asiyeweza kufanya Chochote bila ya Msaada wa mtu mwingine. Mzee kwa sasa hubebwa au kusukumwa na Kiti cha Magurudumu (Wheel Chair) ambayo humsaidia kwa ajili ya kusogezwa eneo moja hadi jingine.

Kwa sasa Mzee huyu anaishi na Mke wake wa 4 Bi. Atusajigwe Mshani wa Mwisho katika wake zake ambaye naye kwa sasa ni mzee mwenye Umri wa miaka 89 licha ya Kuwa ana umri sawa na Mzaliwa  wa tano wa Mzee Ambilikile Panja.

Aidha, kwa mujibu wa mtoto wa Mwisho wa Mzee Panja ambaye ndiye hutunza takwimu za familia ya Mzee Ambilikile, Ndugu Lawrence A. Panja; Baba yake anadhaniwa alizaliwa mwaka 1890 Katika Kijiji cha Kapelekeshi Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.

Kikongwe huyu hajulikani popote zaidi ya Vijiji vinavyo mzunguka. Hata Serikali ya Wilaya tu haijui kuwa ina Raia wake mwenye Umri mkubwa namna hii.
Ni wajibu wetu kama Nchi kusaidia dunia kumfahamu Babu huyu mwenye Umri Mkubwa kuliko wengine. Ni jukumu la Wandishi na Vyombo mbalimbali pamoja na  Mitandao ya Kijamii kuujulisha Ulimwengu Mtu huyu anayeishi maisha ya mwendo wa Marathon kwa sasa.

Sio kila siku tunafuatilia na kusimulia mambo ya Mataifa ya Nje wakati MUNGU na sisi katupendelea. Kama tumeweza kuuambia ulimwengu Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na sio Kenya basi na hili tunaweza tukiamua.

Mwisho naomba Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini Mashirika ndani na nje ya Nchi, pamoja na Wananchi mbalimbali kujitolea kumsaidia na kumtunza Mzee Panja ambaye kwa Umri wake ni kama Lulu iliyosalia Duniani kwa sasa.

Kutoka whatsapp group

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MAKALA : HUYU ULIMWENGU HAUMJUI, HEBU MPELEKENI DUNIANI.
MAKALA : HUYU ULIMWENGU HAUMJUI, HEBU MPELEKENI DUNIANI.
https://2.bp.blogspot.com/-QsDyBAXM9yk/WQB9j9_xISI/AAAAAAAAaG0/dCXUcjmh3B8HcDMUX_2GqZHyr86xALSngCLcB/s1600/IMG-20170426-WA0010.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-QsDyBAXM9yk/WQB9j9_xISI/AAAAAAAAaG0/dCXUcjmh3B8HcDMUX_2GqZHyr86xALSngCLcB/s72-c/IMG-20170426-WA0010.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/makala-huyu-ulimwengu-haumjui-hebu.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/makala-huyu-ulimwengu-haumjui-hebu.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy