MAMA ANNA MGHWIRA ATANGAZA JIMBO ATAKALOGOMBEA UBUNGE 2020

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Mama Anna Mghwira amesema kuwa Tanzania bado haina uchaguzi wa demokrasia huku akiweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 katika jimbo la Singida Mjini.
Mama Anna Mghwira aliyekuwa mwanamke pekee kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu 2015 aliyasema hayo jana Jumatatu Aprili 17, 2017 wakati akizungumza kupitia kipindi Cha Dakika 45 cha ITV.
“Siwazi siioni Tanzania ya uchaguzi ya mwaka 2020. Hatuna chaguzi za demokrasia bado. Pengine naweza kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Singida mjini mwaka 2020,” alinukuliwa Mama Anna Mghwira wakati akieleza mipango yake katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Mama Mghwira ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa alisema kuwa endapo serikali inataka kufanikisha kuwa na uchumi wa viwanda, basi kuna kila sababu ya kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa ili kupata malighafi za kiwandani.
“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya viwanda bila ya kuboresha kilimo kwanza, tunahitaji kuwa na Tanzania ya kilimo kwanza,” alisema.
Jimbo la Singida Mjini kwa sasa linashikiliwa na Mbunge Mussa Ramadhani Sima kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post