MAMBO 7 MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTOA TAARIFA TANESCO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewaomba wateja wake wanaotoa taarifa mbalimbali kupitia kurasa za shirika hilo zilizopo kwenye mitandao ya kijamii kutoa taarifa hizo kwa ufasaha ili kupata ufumbuzi kwa wakati.
Haya hapa chini mambo saba muhimu ya kuzingatia wakati wa kutoa taarifa TANESCO.
1.ENEO HUSIKA
Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti.
2.NAMBA YA SIMU
Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe.
3.KARIBU NA NINI
Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk.
4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO
Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa.
5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI
Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.
6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME
Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77.
7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI
Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk.
TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.
ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post