MANENO YA MBUNGE PETER LIJUALIKALI (CHADEMA) BAADA YA KUTOKA GEREZANI

Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro, Peter Ambrose Lijualikali amesema kuwa ilikuwa ni fahari kwake kukaa gerezani kwa takribani miezi miwili na nusu sababu ya kutetea haki za wanyonge.
Ni heshima kubwa, nimefungwa kwa sababu ya kukataa uchakachuaji. Walinifanyia vurugu halafu baadae wakanigeuzi kesi wakisema mimi ndiye niliyefanya vurugu.
Mbunge huyo wa CHADEMA aliyesema hayo baada ya kuachiwa huru katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam kufuatia Mahakama Kuu kutengua hukumu ya kifungo cha miezi sita aliyokuwa amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.
Mbunge huyo ailisema viongozi wengi wa vyama vya upinzani nchini wamekuwa wakionewa bila kujali nyadhifa na heshima zao kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kubambikiwa kesi kama ilivyokuwa kwake yeye. Alihoji pia, kama Mbunge anaweza kubambikiwa kesi na kufungwa ili matakwa ya baadhi ya watu yatimie, itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida?
Mahakama Kuu iliamuru kuachiliwa kwa mbunge huyo aliyefungwa kwa kosa la kufanya vurugu kwenye uchaguzi baada ya kubaini mapungufu katika hati ya mashtaka ya kiongozi huyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post