MANENO YA MKE YA ROMA MKATOLIKI KWA WALIOMTEKA NA KUMTESA MUME WAKE

Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza tokea mume wake alipotekwa na kupatikana akiwashukuru Watanzania wote ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi hicho kigumu.
Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo hayo.
“Yeremia 30:16-17:- Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.
Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru watanzania wote ambao wamesimama pamoja nao katika kipindi hiki kigumu alichokipitia Roma.
“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.
Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukiohilo ili kupata ripoti kamili na wahusika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post