MAROUANE FELLAINI ATOLEWA NJE KWA KADI WAKATI MAN U NA MAN CITY ZIKITOKA SARE

Marouane Fellaini ametolewa nje ya uwanja kwa kumpiga kichwa Sergio Aguero wakati timu za Manchester City na Manchester United ambao ni mahasimu wakuu wa Jiji la Manchester wakipambana na kutoka sare tasa katika dimba la Etihad Stadium.

Matokeo hayo yamemuacha kocha Manchester United, Jose Mourinho, akiwa na furaha kwa kufikisha michezo 24 bila ya kufungwa, mafanikio ambayo yamefikiwa licha ya Fellaini kutolewa nje ya uwanja kwa kufanya kitendo hicho cha kizembe.

Mchezaji raia wa Argentina Aguero nusura afunge lakini shuti lake liligonga mwamba huku kocha wao Pep Guardiola akimaliza mchezo huo akiwa na hofu ya kipa wake Claudio Bravo kupata jeraha na kuondolewa kwa kubebwa kwenye machela.
Marouane Fellaini akimwangalia Sergio Aguero akianguka chini baada ya kumpiga kichwa
               Marouane Fellaini akipewa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Sergio Aguero

        Sergio Aguero akishika kichwa akishindwa kuamini baada ya kukosa goli la wazi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post