MATOKEO YA MCHEZO KATI YA SERENGETI BOYS NA GABON

Timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 imeendelea kujiwinda vyema na michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCONU-17) baada ya leo kupata ushindi dhidi ya wanaotarajiwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Mei 14 mwaka huu.
Serengeti Boys imeshuka dimbani leo saa 10 jioni kwa saa za Morocco ambapo imecheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Gabon na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Serengeti Boys ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kabla ya Gabon kusawazisha na hivyo kwenda mapumziko wakiwa moja moja. Katika kipindi cha pili, Serengeti Boys walipata goli jingine na hivyo kujiandikia ushindi wao wa kwanza wa 2-1.
Serengeti Boys watacheza mchezo mwingine wa Kirafiki wakiwa Morocco kabla ya kuelekea Cameroon ambapo watacheza michezo miwili ya kirafiki na kisha kwenda Gabon kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post