MBUNGE ATUHUMIWA KUINGIA NA ‘MZINGA’ WA KONYAGI BUNGENI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amemtuhumu Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari kuwa alitaka kuingia katika eneo la bunge akiwa na chupa ya konyagi.
Tuhuma hizo za Waziri Mwakyembe zimekuja wakati wabunge hao wawili ulioanza jana katika ukumbi wa bunge ambapo Nassari alisema Waziri Mwakyembe amekuwa akitoa maamuzi yake kwa upendeleo na kwamba ni kiongozi aliyekosa msimamo.
Nassari aliyasema hayo wakatika akichangia hotuba ya bajeti ya TAMISEMI ambapo alisema Mwakyembe hana msimamo kwani aliongoza kamati ya Richmond ya mwaka 2008 iliyomuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa bila hata kupewa nafasi ya kujitetea, na sasa anaongoza Wizara ya Habari lakini hataki RC wa Dar es Salaam ahojiwe kwa tuhuma zinazomkabili.
Nassari alisema pia katika andiko la Mwakyembe la Shahada ya Uzamivu (PhD) aliandika kupendekeza serikali tatu za muungano lakini alipokuja kwenye Bunge la Katiba Mpya alikuwa akitetea serikali mbili.
Akijibu tuhuma za kutaka kuingia na mzinga wa konyagi ndani ya eneo la bunge, Joshua Nassari amesema jambo hilo halina ukweli na ni la kupuuzwa.
Mbunge Joshua Nassari ameyasema hayo mapema leo wakati akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge baada ya Waziri Mwakyembe kutoa tuhuma hizo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post