MSANII WA UFARANSA AATAMIA MAYAI YA KUKU

Msanii wa Ufaransa, Abraham Poincheval amefanya tukio hatarishi la kuiishi ndani ya chumba maalum kwa lengo la kutotoa vifaranga wa kuku akitumia joto la mwili wake.
Atakaa kwa muda wa wiki tatu (siku 21 mpaka 26) katika chumba maalum cha vioo akiatamia mayai kumi ya kuku kwa kutumia joto la mwili wake. Watalii wengi wamekuwa wakimuangalia msanii huyo ambaye mpaka sasa ameshatumia muda wa wiki tatu akiwa ndani ya chumba hicho katika makumbusho ya Palais de Tokyo nchini Paris.
“Ukweli ni kuwa nitakuwa kuku” alisema.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 44 alianza tukio hilo alilolipa jina la  “Oeuf” lenye maana ya “Mayai” siku ya jumatano ya Machi 15, 2017. Aliyakalia mayai hayo katika kiti kilichowekewa mfuko chini yake.
Poincheval amejifunga blanketi ili kuzuia joto kupotea na anatumia vyakula vinavyoongeza sana joto mwilini kama vile tangawizi.
Wakati wa haja, msanii huyo hatopaswa kuinuka kwenda kujisaidia, badala yake atatumia boksi maalumu lililotengenezwa chini ya kiti hicho.
Ili mayai yaweze kuanguliwa vizuri, anapaswa kuinuka katika kiti hicho kwa muda usiozidi dakika 30 ndani ya saa 24.
Kabla ya kufanya tukio hilo la kuatamia mayai ya kuku, Poincheval amewahi pia kuishi ndani ya jiwe la chokaa lililotengenezwa kwa umbo la yai.
French artist Abraham Poincheval poses inside his artwork Pierre (
Amewahi pia kuishi ndani ya sanamu ya dubu, katika mfereji ulioko chini ya maktaba na kusafiri ndani ya maji akiwa katika chupa kubwa ya plastiki iliyowekwa mfuniko.
French artist Abraham Poincheval climbs into a fake bear on 31 March 2014 the day before starting an artistic performance in which he will spend 13 days in the bear's skin, at the Hunting and Wildlife Museum in Paris
French artist Abraham Poincheval poses on 20 September 2012 in Marseille, southern France, before starting his artistic performance 604.800 seconds.
French artist Abraham Poincheval stands in a giant bottle during his performance The Bottle' 30 July 2015 in Port-Saint-Louis-du-Rhône, southern France

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post