MTOTO WA MIEZI 9 ASHTAKIWA KWA MAUAJI NCHINI PAKISTAN

Mtoto mwenye umri wa miezi 9 amefikishwa mhakamani nchini Pakistan na kushtakiwa kwa makosa ya kupanga mauaji, kutishia polisi na pia kuzuia shughuli za serikali.
Muhammad Mosa Khan alikamatwa mwezi Februari mwaka huu pamoja na watu wengine 30 wakiwepo ndugu wa familia yake. Mtoto huyo pamoja na wenzake waliokamatwa wanatuhumiwa kutaka kuwaua maafisa wa polisi kwa kuwapiga kwa mawe walipokuwa na maafisa wa shirika la umeme la nchini humo wakifaanya ukaguzi katika Mji wa Lahore ambao wakazi wake wamekuwa wakituhumiwa kutumia umeme bila kulipia.
Afisa wa Polisi Kashif Ahmed alimkamata mtoto huyo pamoja na familia nzima ya Muhammad Yaseen akiamini kuwa alikuwa na uwezo na alishiriki katika tukio hilo la kuwarushia mawe polisi.
Wakiwa mahakamani mtoto huyo alichukuliwa alama za vidole kisha akakaa kwenye mapaja ya babu yake akionekana kutoelewa chochote kilichokuwa kikiendelea katika chumba cha mahakama.
Baada ya mashtaka hayo watuhumiwa wote walipewa dhamana na walirejea tena mahakamani Aprili 12 mwaka huu. Jaji anayeendesha keshi hilo alikiri kuwa haikuwa ya kawaida sababu ya kumhusisha mtoto mwenye umri mdogo, lakini hakuwa na mamlaka ya kufutia kesi.
Babu wa mtoto huyo, Mohammad Yaseen aliliambia shirika la habari la Reuter kuwa, alishangazwa na kitendo cha mjukuu wake kukamatwa na kujumuishwa katika kesi hiyo kwani mwenyewe hawezi hata kushika vizuri chupa yake ya maziwa, sasa kwa vipi angewapiga polisi kwa mawe?
Inspekta wa Polisi Msaidizi, Kashif Ahmed alisimamishwa kazi kwa kumkamata mtoto huyo, na pia mamlaka husika zimesema zitawachukuliwa hatua wote walioshiriki kuandikisha kesi dhidi ya mtoto huyo.
Mtoto ambaye yupo chini ya umri wa miaka 7 hawezi kushtakiwa kwa kosa lolote kwa mujibu wa sheria ya adhabu ya Pakistan.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post