MTU MMOJA AKAMATWA KWA WIZI WA MBEGU ZA KIUME

Polisi nchini Thailand wamemkamata mwanaume mmoja akijaribu kuingiza kwa njia za magendo vichupa sita vyenye mbegu za kiume za binadamu nchini Laos.
Mamlaka za Thailand zilibaini chupa kubwa ya gesi ya Nitrogeni kwenye begi la Nithinon Srithaniyanan, (25) ikiwa na vichupa hivyo wakati akitaka kuvuka mpaka katika Mji wa Nong Khai uliopo Kaskazini mwa Thailand.
Polisi wamesema mwanaume huyo amethibitisha kuwa vichupa hivyo vilikuwa na mbegu za kiuume kwa ajili ya kiliniki ya tiba utungaji mimba Jijini Vientiane nchini Laos.
Polisi walithibitisha kuwa mbegu hizo za kiume ni za wanaume kutoka China na Vietnam, na mwanaume huyo alisema kuwa amefanya safari za kuvuka mpaka mara 12 kwa mwaka jana pekee akichukua mbegu hizo kutoka Bangkok kupeleka Laos.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post