MUIGIZAJI LULU AKANUSHA TAARIFA ZA KUFUNGA NDOA

Hivi karibuni magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yameandika taarifa kuwa muigizaji Lulu amesema kuwa ndoa yake na mpenzi wake Fransic Shiza maarufu kama Majay ambaye pia ni bosi wa EFM na TVE inakaribia.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter, Lulu amekanusha taarifa hizo kwa kuandika, “Hivi kwa Akili yenu Ndoa inatangazwaga Kwenye Magazeti!??Muwege mnajiongeza kabla ya kuparamia Story…!.” Kauli hii imekuja kufuatia habari ya gazeto la Mwananchi la leo Aprili 18, 2017 kuwa Lulu alisema ndoa yake inakaribia na angependa kuwa na ndoa bora kama yalivyo mapenzi yake.
Kwenye gazeti la Mtanzania la siku chache zilizopita, lilinukuu kauli ya muigizaji huyo aliyodaiwa kusema, “Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post