MVUA ZA SABABISHA MAFURIKO, WANANCHI WAKOSA PA KULALA

Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha madhara makubwa kwa wananchi wa Chalinze baada ya kutokea mafuriko ambapo takribani nyumba kumi zimesombwa na maji
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze,  Ridhiwani Kikwete amesema kuwa uharibifu ulijitokeza ni mkubwa hivyo wananchi hao waliokumbwa na tatizo hilo wanahitaji msaada wa dharula.
Aidha, Ridhiwani ametaja maeneo yaliyoathirika na mvua hizo ambazo zimesababisha mafuriko ni Chalinze Mzee, Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.
Hata hivyo, ameongeza kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba, nyumba za wananchi kuharibika na kusabishwa wananchi kukosa pa kulala hivyo amesema wananchi hao wanahitaji kusaidiwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post