NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR, DR. ABDULLA JUMA ABDULLA ( MABODI ) ATAMBULISHWA MAHONDA

SHARE:

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Abdulla { Mabodi } akizungumza na Viongozi wa CCM Ngazi ya Shina hadi Wilaya ya Kaskaz...

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Abdulla { Mabodi } akizungumza na Viongozi wa CCM Ngazi ya Shina hadi Wilaya ya Kaskazini “B” wakati akijitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni hapo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Jimbo la Mahonda iliyopo Kinduni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa kushoto akimpa agizo Mkuu wa Kituo cha Polisi Mahonda kuchunguza Watu waliochukuwa baadhi ya vyarahani vya mradi wa mafunzo ya Vijana kwenye Ofisi ya Jimbo la Mahonda Kinduni.

Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Abdulla { Mabodi } NA Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Nd. Juma Haji Juma.

Mmoja wa Viongozi wa CCM ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Almas Jamal Ramdhan akichangia kwenye Mkutano huo wa kutambulishwa kwa Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CCM Zanzibar Dr. Mabodi hapo Kinduni.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Mahonda na Timu yake kufanya uchunguzi wa kuwabaini watu waliohusika na upotevu wa baadhi ya vyarahani vilivyokuwa vikitumiwa na Vijana katika mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wa ajira ndani ya Ofisi ya CCM Jimbo la Mahonda hapo Kinduni Wilaya ya Kaskazini “B”.

Aliagiza uchunguzi huo uende sambamba na watakaohusika na wizi huo kuwekwa ndani kwa muda wa siku tatu na baadae taratibu za kisheria za kuwafungulia mashtaka zifuatwe kutokana na kitendo chao kiovu cha ukosefu wa nidhamu na maadili.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa kutambulishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Abdulla {Mabodi } mbele ya Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Shina hadi Wilaya ya Kaskazini “B” hapo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Jimbo la Mahonda Kinduni.

Akiwa Mbunge wa lililokuwa Jimbo la Kitope Mwaka 2010 hadi 2015 alilazimika kutumia maarifa na nguvu zake nyingi kuanzisha mradi wa Vyarahani 30 uliolenga kutoa mafunzo ya ufundi kwa Vijana wa Jimbo hilo ili kuwapa uwezo wa kujitegemea kimaisha kwa vile fursa za ajira Serikalini kwa sasa zimepungua.

Alisema inasikitisha na kutia uchungu kuona baadhi ya Watu wameufanyia dhihaki mpango huo kwa kufikiria zaidi maslahi na mahitaji yao binafsi jambo alisema halikubaliki kabisa kwa vile linarejesha nyuma maendeleo ya Vijana walio wengi katika maeneo hayo ambao idadi yao inaongezeka kila mwaka baada ya kumaliza masomo yao.

Balozi Seif Ali Iddi amempa Mkuu wa Kituo hicho cha Polisi Mahonda kipindi kifupi cha kukamilisha uchunguzi huo na kuwasilisha ripoti ya uchunguzi huo kwake huku taratibu za kuwapeleka mahakamani zikiendelea ili kuwabaini wabadhirifu hao wa mali na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya Jamii.

“ Tulilazimika kutafuta Walimu kutoka Sehemu mbali mbali hapa Zanzibar kwa ajili ya kuwafundisha Vijana wetu kazi za Ufundi ili waweze kujitegemea lakini wenzetu waliona mchezo “. Hili halikubaliki kabisa. Alisisitiza Mwakilishi huyo wa Jimbo la Mahonda.

Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi alimpongeza Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Abdulla { Mabodi } kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Balozi Seif alimuahidi Dr. Mabodi kuwa Uongozi wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” umemuhakikishia kumpa ushirikiano wa karibu katika kuona utekelezaji wa majukumu yake aliyokabidhiwa unakuwa mzuri na kuleta ufanisi mkubwa.

Mapema akizungumza na Viongozi hao wa CCM Kunazia ngazi ya Shina hadi Wilaya ya Kaskazini “B” Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdulla Juma Mabodi aliwatahadharia wana CCM kuwa makini na Watu waliojitoa mshipa wa fahamu kuanza kutengeneza safu ya Uongozi wakijiandaa na uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Dr. Mabodi alionya kwamba kitendo hicho kilicho nje ya sheria kanuni na taratibu za Chama kamwe hakikubaliki kabisa wakati huu mbao Wananchi wanategemea kupata maendeleo kutoka Viongozi waliowachagua ndani ya kipindi cha sasa cha miaka Mitano.

Alipendekeza kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya shina kuwachagua wanachama wenzao wanaouzika kutokana na ushawishi mkubwa walionao na kuachana na wale wanaotaka madaraka kwa kutumia uwezo wa kifedha.

“ Mtaji wa Chama ni Wanachama wenyewe. Hivyo hata mkichagua Mama Lishe, Mchuuzi wa Samaki na muuza karanga iwapo anakubalika na jamii iliyomzunguuka basi mpeni ridhaa akutumikieni “. Alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar.

Dr. Mabodi alieleza wazi kwamba Vyama vya TANU na ASP vilivyozaa Chama cha Mapinduzi vimetengeneza msingi imara na mizuri ya kupata Viongozi makini na wigwa na wana CCM wa Kizazi kipya ili kurejesha heshima ya Chama hicho kilichozaa Tanzania Mpya.

Akizungumza zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kujiandaa kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi ndani ya CCM Dr. Mabodi alisema alilazimika kuongeza muda wa saa 48 za uchukuaji wa fomu ili kuwapa fursa Wanachama wa CCM kutumia haki yao ya Kidemokrasia.

Alisema yapo malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya Wanachama wa CCM kufanyiwa mahojiano wakati wa uchukuwaji wa fomu hizo kitendo ambacho wanaelewa kuwa ni kinyume na kanuni na utaratibu wa Chama.

Aliwaonya Viongozi na watendaji wanaosimamia zoezi hilo kuacha mara moja tabia hiyo inayoashiria cheche ya rushwa katika kupanga safu ya Uongozi mambo yaliyopigwa mstari mwekundu ndani ya CCM Mpya isidita kuwafyeka mara moja watu hao ikibaini kuhusika na vitendo hivyo.

Akichangia kwenye Mkutano huo Mmoja wa Viongozi hao wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Almas Jamal Ramadhan alisema wakati huu Wana CCM wanahitaji Wanasiasa watakaokuwa makini kuchapa kazi ili kwenda sambamba na CCM Mpya iliyozaa Tanzania Mpya.

Nd. Jamal alisema kuendelea kutegemea Viongozi wa Kisiasa kipindi hichi ni sawa na kukirejesha Chama cha Mapinduzi { CCM } ndani ya dimbwi la mazonge wakati tayari k imeshajisafisha kujiendesha katika uwajibikaji wa Kitaalamu zaidi.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
16/4/2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR, DR. ABDULLA JUMA ABDULLA ( MABODI ) ATAMBULISHWA MAHONDA
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR, DR. ABDULLA JUMA ABDULLA ( MABODI ) ATAMBULISHWA MAHONDA
https://4.bp.blogspot.com/-DBs0b5dX2Zg/WPSlJNm6G9I/AAAAAAAAZos/gesjoeuN94MdANj_HJK3ZtKXHtMbpvutACLcB/s1600/AJO%2B1.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-DBs0b5dX2Zg/WPSlJNm6G9I/AAAAAAAAZos/gesjoeuN94MdANj_HJK3ZtKXHtMbpvutACLcB/s72-c/AJO%2B1.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/naibu-katibu-mkuu-wa-ccm-zanzibar-dr.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/naibu-katibu-mkuu-wa-ccm-zanzibar-dr.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy