NAMNA YA KUMVUTIA MTEJA KATIKA BIASHARA YAKO

Unapoanzisha biashara na kupata wateja, kazi kubwa inayofuata ni kuhakikisha wateja wako unaendelea kuwa nao. Yaani wanaendelea kufanya biashara na wewe.
Ni rahisi sana kufanya biashara na mteja uliyewahi kuwa naye kibiashara kuliko mteja mpya. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwafikisha wateja kwenye biashara zao, lakini wanapofika na kupata huduma kwa mara ya kwanza huondoka na wengi wao huwa hawarudi tena.
Lakini wewe mfanyabiashara unapoweza kuiendesha biashara yako vizuri, wateja wanaonunua kwako, wanaweza kuwa wako milele.
Zifauatazo ni mbinu unazoweza kuzitumia kwenye biashara yako ili kuhakikisha wateja wako wanaendelea kufanya biashara na wewe.
Kama umemtangazia mteja wako kwamba akija kwenye biashara yako atapata kitu fulani, basi hakikisha anapata kitu hicho. Hakuna kitu wasichopenda watu kama kudanganywa. Mteja anapoona kwamba umemdanganya, ni vigumu kurudi tena. Ni bora kuahidi kidogo ukatekeleza kuliko kuahidi usitekeleze.
Ni muhimu kwa mfanyabiashara yeyote kuwa na mawasiliano na wateja wake. Bila kujali ni biashara gani unafanya, ikiwezekena jitahidi kupata namba za simu au barua pepe za wateja wako. Mara kwa mara watumie ujumbe ukiwatakia heri, mfano mwaka mpya au sikikuu nyingine yoyote ile kubwa, na wakati mwingine ukiwajulisha bidhaa au huduma mpya zilizoko kwenye biashara yako.
Jitahidi sana kuyatatua matatizo ya wateja wako endapo wanakuwa na malalamiko. Yafanyie kazi kwa haraka wajione unawajali, usisubiri mpaka yawe makubwa kiasi cha kuwafanya watafute mahali pengine.
Huduma kwa mteja ni pampja na namna ya kumpokea, jinsi ya kumueleza juu ya bidhaa au huduma anayohitaji na jinsi ya kumjibu maswali yake. Hivi ni  vitu vinavyoweza kuonekana kuwa ni vidogo, lakini vina maana kubwa kwa wateja.
Hakikisha wateja wako wanapata huduma (Customer service) ambazo zinawafanya wajisikie wafalme.
Kama biashara yako ni ya muda mrefu, lazima kuna baadhi ya wateja waliokuwepo awali waliopotea. Ni vyema kuwatafuta ikiwezekana, kujua sasa wanafanya biashara na nani na ni kitu gani kilichowafanya wasije tena kwako.
Unapompata mteja hakikisha unamdadisi kama ana kitu kingine zaidi anbacho angehitaji, lakini hakikuwa kwenye bajeti yake, na kipo kwenye biashara yako.
Ni jukumu lako kujua mahitaji haya yote na kuyafanyia kazi.
ussishie kumuuzia mteja kitu kimoja tu alicholenga kununua. Kama biashara yako inahusisha wateja kwenye mitandao, hakikisha unaitangaza kwenye mitandao, na ikiwezekana kuwa na tovuti au blogu au kurasa kwenye mitandao ya kijamii.
Vilevile jitahidi kuwa na njia ya kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wa kudumu, au wale wanaorudi tena kwenye biashara yako. Unaweza kuwapatia kuponi ya punguzo kadiri wanavyonunua mara nyingi, au kutoa punguzo la bei kwa mteja kama ananunua mara nyingi kwa idadi kubwa.
Kwa vyovyote vile hakikisha mteja anapata motisha pale anaponunua kwako kwa muda mrefu. Anza kazi hiyo ili kuboresha uhusiano wako na wateja ili uweze kukuza biashara yako.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post