NAY WA MITEGO: USALAMA WA MAISHA YANGU UPO HATARINI

Mwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amesema kuwa usalama wa maisha yake kwa sasa ni mdogo sana kutokana na baadhi ya watu kumtisha kutaka kumuua.
Nay wa Mitego ambaye siku za hivi karibuni alikuwa matatizoni kutokana na wimbo wake wa WAPO ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa yeye ni msanii na anachofanya ni muziki si mambo mengine hivyo hawezi kutishika.
Aidha, Nay amesema kuwa licha ya kuwa anakumbana na vitisho vyote hivyo hawezi kuhama nchi wala kukimbilia popote na kwamba ataifia hapa hapa nchini;
“Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea,” aliandika Nay.
Aliandika pia, “Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod🙏🏿#Wapo #Truth.”


Kauli hii ya Nay wa Mitego imekuja siku moja baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kusema kuwa amekuwa akitumiwa jumbe za vitisho kuwa atauwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post