NDALICHAKO ATETEA MAKATO YA VYUO VIKUU

WAKATI kukiwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi walionufaika na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuwa makato ya asilimia 15 ya mshahara kabla ya kodi kama marejesho ni makubwa-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema makato hayo yapo kwa mujibu wa sheria.
Amesema hakuna jambo ambalo serikali inafanya bila kufuata sheria hivyo makato hayo yapo kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Tangu Novemba 14, mwaka jana Serikali ilipopitisha sheria mpya ya kulipa mikopo kwa wahitimu wa elimu ya juu kutoka asilimia nane hadi 15, kumekuwapo na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi, ikiwamo pia kutoka Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (Tucta) kuhusu makato hayo.
Tucta waliitaka Serikali kusitisha makato hayo na kurudia kiwango cha awali kinyume na hapo wataipeleka mahakamani.
Juzi, Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya Bajeti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017/18, Waziri Ndalichako alitolea ufafanuzi suala hilo baada ya Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya kuhoji uhalali wa Serikali kukata makato hayo.
Akijibu hoja hiyo, Prof Ndalichako alisema hakuna jambo ambalo Serikali inafanya kinyemela bila ya kufuata sheria.
Alisema utaratibu wa kuwakata waajiriwa waliokuwa wanufaika wa HESLB ulianza kwa marejesho ya Sh. 50,000 kwa mwezi lakini mwaka 2011 waziri mwenye dhamana akaanzisha utaratibu wa kukata asilimia nane ya mshahara kwa siku hizo.
“Utaratibu huu haukuwapo awali kwani walikuwa wanakatwa Sh 50,000 kwa mwezi na ilipofika mwaka 2011, waziri mwenye dhamana akaanzisha utaratibu kwa kuwakata asilimia nane ya mshahara anaopewa mwajiriwa na sasa utaratibu umeingizwa kwenye sheria na mwaka jana tukakubaliana na HESLB makato yawe asilimia 15,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema Serikali inafanya makato hayo kwa lengo la kuwawezesha watoto wengine wa kitanzania ambao hawana uwezo wa kujisomesha vyuo vikuu nao waweze kunufaika.
Wakati akichangi bajeti hiyo, Sakaya aliihoji Serikali kwanini wanawakata watumishi asilimia 15 kama malipo ya mkopo wa elimu ya juu kinyume na makubaliano.
“Makato hayo ni kinyume na makubaliano, naomba kauli ya Serikali kuwa kwanini wanawakata asilimia 15 badala ya asilimia nane kwa sababu hii asilimia ni nyingi sana ikilinganishwa hali ya uchumi wa sasa,”alisema Sakaya.
Alisema Serikali inapaswa kupunguza asilimia hiyo kwa sababu makato hayo yanawaumiza wafanyakazi kulinganisha na bei ya vyakula na hali ya maisha kuwa ngumu
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post