NINASUBIRI RIPOTI YA WATUMISHI WA SERIKALI WENYE VYETI FEKI NIIFANYIE KAZI- RAIS MAGUFULI

Ninafahamu changamoto za walimu wa hapa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mazingira ya kufundishia naelewa kuwa ni magumu kwa sababu hata mimi nimesoma hapa, lakini pia hata maslahi yenu nafahamu kuwa ni madogo lakini nawaomba muendelee kuwa fundisha hawa vijana.
Ninawaomba mvumilie kidogo hadi hapo nitakapopatiwa ripoti ya watumishi wa serikali tutaweza kushughulikia changamoto zenu. Ripoti hiyo inachunguza pia watumishi ambao wana vyeti feki ambao naambiwa ni takribani 9,000.
Hayo yamesemwa na Rais Dkt Magufuli mapema leo asubuhi alipokuwa akifungua rasmi nyumba mpya za makazi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambazo aliahidi kuwa angezijenga alipokuwa chuoni hapo mwaka jana.
Rais Magufuli amefungua hostels hizo zenye uwezo wa kubeba wanafunzi zaidi ya 3800 na zimegharimu TZS bilioni 10 zikiwa zimejengwa kwa muda wa miezi minane.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Rais Dkt Magufuli alisema kuwa atakapopokea ripoti hiyo ya watumishi wa serikali ndipo ataweza kutambua hasa changamoto zinazowakabili na kuweza kuzitatua. Lakini pia ripoti hiyo itaweza kubaini wafanyakazi waliofanya udanganyifu kwa kughushi vyeti na kupata ajira serikalini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post