NIYONZIMA ANENA KUELEKEA PAMBANO LAO DHIDI YA AZAM FC

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima,amesema kuwa  anaamini timu yake inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ni lazima leo Jumamosi iifunge Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga na Azam tangu mwaka 2008, zimekutana mara 17 katika ligi kuu na zote zimeshinda mechi tano kila moja na zimetoka sare mara saba. huku Yanga imefunga mabao 23 na Azam imefunga mabao 22.
Aidha, Katika msimamo wa ligi kuu, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 53 nyuma ya Simba iliyopo kileleni kwa pointi 55, Azam ni ya tatu na pointi 44.
Niyonzima ambae ni raia wa Rwanda, amesema mchezo huo utakuwa mgumu kulingana na historia yao kila wanapo kutana lakini kwao ni muhimu kwani wakishinda watakuwa na mwanga mzuri wa kutwaa ubingwa.
 “Mechi yetu na Azam ni mchezo mkubwa na utakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila upande unahitaji ushindi, lakini tumejipanga kushinda kwani ndiyo mechi ambayo itatoa mwelekeo wa kutetea ubingwa wetu,”amesema Niyonzima.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post