OZIL AITAKA ARSENA WAJIFUNZE KUPITIA HILI

Kiungo mjerumani Mesut Ozil anaekipiga kunako klabu washika bunduki  Arsenal The Gunner ameonekana bado anaumizwa na kitendo cha timu hiyo kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kipigo cha aibu kutoka kwa Bayern Munchen ya nchini Ujerumani.

Hivi karibuni nyota huyo alifunguka na kusema “Arsenal kama timu na sisi wachezaji lazima tujifunze kupitia kipigo kikubwa na cha aibu tulichofungwa dhidi ya wapinzani wetu kwenye Ligi ya Mabingwa hilo litasaidia kwa sisi wachezaji kuendelea kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kuhakikisha tunalinda heshima yetu wachezaji na klabu kwa ujumla.”

Ikumbukwe Arsenal sasa ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza na kesho jumatatu wanakibarua kizito kwa kucheza na wenyeji wao Middlesbrough kwenye muendelezo wa Ligi kuu nchini humo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post