PICHA 11: HOTELI YA TARIJI MWINGINE KUPIGWA MNADA NA BENKI YA EXIM JUMAMOSI

Benki ya Exim inatarajia kupiga mnada hoteli ya kifahari ya Slim Slim pamoja na samani za kumbi za mikutano vilivyopo Bagamoyo mkoani Pwani baada ya mmiliki huyo kushindwa kurejesha mkopo wa TZS 920 milioni.
Benki ya Exim inatarajia kufanya mnada wa hoteli hiyo maarufu ya Green Park Village siku ya Jumamosi Aprili 22 mwaka huu ambapo watahitaji TZS 2.5 bilioni lakinim mmiliki wa hoteli hiyo amesema kuwa thamani ya hoteli hiyo ni TZS 5 bilioni na si bei iliyotajwa na benki. Wakazi wa eneo hilo wanaombea hoteli hiyo iuzwe kwa thamani halisi ili mmiliki huyo aweze kupata fedha za kuendeshea maisha yake kwani hatobakiwa na kitu kingine.
Gazeti la The Citizen limemnukuu Slim Slim mmiliki wa hoteli hiyo akisema kuwa, anaamini Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itaingilia sakata hilo ili kuweza kunusuru hali ngumu anayopitia yeye kama mwekezaji kwani serikali iliwaahidi wawekezaji mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Alisema Hoteli ya Green Park Village ni ndoto yake aliyokuwa nayo siku nyingi tangu alipokuwa akiishi nchini Norway. Hoteli hiyo ina vyumba vya kulala 20, vyumba 7 vya mikutano, na sehemu mbili za mapumziko.
“Niliuza kila kitu nilichokuwa nikimiliki nchi Norway na kuamua kurejea nchini mwangu baada ya serikali kutushawishi wazawa tuliopo nje ya nchi tushiriki katika maendeleo ya nchi yetu.” 
Slim alisema kuwa alikopa benki hiyo TZS 894 milioni miaka mitatu iliyopita akitakiwa kulipa na riba ya asilimia 10, na ilipofika mwaka jana alishindwa kulipa deni hilo.
Sakati hili la mali kupigwa manada halijamkumba Slim Slim peke yake, kwani Benki ya Exim leo inatarajia kupiga manada Peninsula Apartments  zilizopo Msasani jijini Dar es Salaam kwa gharama ya TZS 11.4 bilioni.
Haikuweza kufahamika mara moja kuwa mmiliki wa nyumba hizo alikuwa akidaiwa kiasi gani na benki hiyo.
Hapa chini ni picha za hoteli hiyo iliyopo Bagamoyo.
Image result for Green Park Village BagamoyoRelated imageImage result for Green Park Village BagamoyoRelated image

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post