PICHA: RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NA BALOZI WA ISRAEL HAPA NCHINI

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja w...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2017 amefanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Roeland Van de Geer na kuushukuru umoja wa nchi hizo kwa kutoa msaada wa Euro Milioni 205 sawa na takribani Shilingi Bilioni 500 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo hapa nchini kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu.
Mhe. Rais Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo kumethibitisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na kwamba pamoja na kutoa fedha hizo umoja huo unatarajia kutoa fedha nyingine kiasi cha Euro Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuendeleza viwanda, kilimo na uzalishaji wa nishati.
“Nimefurahi sana kwamba uhusiano na ushirikiano wetu unajikita kushughulikia mambo ya msingi kwa Watanzania, nakuhakikishia kuwa fedha mnazotoa zitatumika vizuri na zitatoa mchango mkubwa katika maendeleo yetu” amesema Mhe. Dkt. Magufuli.
Nae Mhe. Balozi Roeland Van de Geer amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi wake mzuri na dhamira yake ya kujenga uchumi na kusimamia utawala bora ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, na pia amemuahidi kuwa nchi wanachama wa umoja huo zitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Tanzania.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan na kumhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani katika masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za kijamii.
Mhe. Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba Mhe. Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini.
“Naamini uhusiano na ushirikiano wetu utaongeza manufaa zaidi kwa nchi zetu na watu wake, nimefurahishwa sana na taarifa kuwa watalii wataanza kuja kwa ndege moja kwa moja kutoka Tel Aviv Israel na hivi karibuni ndege yenye watalii zaidi ya 200 itakuja nchini kwetu, nawakaribisha sana watalii na wawekezaji kutoka Israel”amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Balozi Yahel Vilan pamoja na ujumbe wake amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa wamefurahishwa na ziara waliyoifanya hapa nchini iliyowawezesha kukutana na viongozi mbalimbali na ameahidi kuwa Serikali ya Israel itajenga jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkoani Dodoma kuanzia mwishoni  mwa mwaka huu.
Mhe. Balozi Yahel Vilan amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa Israel itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha huduma za matibabu kwa wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan baada ya kutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Roeland Van de Geer alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Roeland Van de Geer alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam April 6, 2017
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Aprili, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: PICHA: RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NA BALOZI WA ISRAEL HAPA NCHINI
PICHA: RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NA BALOZI WA ISRAEL HAPA NCHINI
https://1.bp.blogspot.com/-YIk8xyPRyFE/WOZtAt1NRrI/AAAAAAAAZJs/xzYcd3Lr9Xg3hPJgkfUCYwRyUyGL3VVewCLcB/s1600/xmagu-750x375.jpg.pagespeed.ic.bLGNEGkzFS.webp
https://1.bp.blogspot.com/-YIk8xyPRyFE/WOZtAt1NRrI/AAAAAAAAZJs/xzYcd3Lr9Xg3hPJgkfUCYwRyUyGL3VVewCLcB/s72-c/xmagu-750x375.jpg.pagespeed.ic.bLGNEGkzFS.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/picha-rais-magufuli-afanya-mazungumzo.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/picha-rais-magufuli-afanya-mazungumzo.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy