PICHA ZA GARI JIPYA LA KIFAHARI ALILONUNUA DIAMOND PLATNUMZ AFRIKA KUSINI

Mwanamuziki Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania leo ameonyesha gari lake jipya la kifahari alilolinunua kwa ajili ya shughuli zake akiwa nchini Afrika Kusini.
Diamond ambaye familia yake (mpenzi wake na watoto wawili) wanaishi nchini Afrika Kusini amechapisha picha za gari aina ya Hammer kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kwamba ni kwa ajili ya shughuli za hapa na pale akiwa Afrika Kusini.
“Jus decided to get this for my south africa’s up and downs trip…..๐Ÿ‘ #SideChick


Baada ya muda mfupi, aliweka picha nyingine ambayo aliambatanisha na ujumbe wa mahaba kwenda kwa mpenzi wake, Zari The Boss Lady anayeishi naye nchini humo.
Diamond aliandika ujumbe unaosomeka kidogo changu mimi nawe, kikubwa cha Barabuu… Mali zao zisifanye upagawe ukaniweka Roho yuu…. so proud to have you mama, tukutane kwenye kuliwakilisha Taifa kwenye Mashuka leo๐Ÿ˜Š @zarithebosslady


Kabla Diamond hajanunua gari hili aliwahi kusema kuwa gari ambalo anapenda kuwa nalo ni Rolls Royce ambalo nalo pia ni miongoni mwa magari ya kifahari zaidi duniani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post