POLEPOLE AITAKA CCM IMUADHIBU NAPE NNAUYE KWA KAULI ALIYOTOA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amelaani vikali kauli iliyotolewa na mtangulizi wake ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa alisaidia kukitoa chama hicho shimoni.
Nape alitoa kauli hiyo dakika chache baada ya mkutano wake na waandishi wa habari kuzuiwa na kutishiwa bastola na mtu mmoja, siku moja baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Polepole ambaye alipokea kijiti kutoka kwa Nape Nnauye, akiwa katika ofisi za Mwananchi Communication Ltd alisema kuwa, kama Nape alitoa kauli hiyo alikuwa amekengeuka. CCM ni chama kikubwa kuliko vyote Afrika, hivyo hakiwezi kuokolewa na mtu mmoja.

“Mwanachama anayejitambua hawezi kusema anakibeba chama, wanachama wote milioni nane walikuwa wapi? Viongozi wote maelfu walikuwa wapi? Nape ni kiongozi wetu kwenye chama, kama kweli alisema maneno hayo alikengeuka sana,” Polepole anakaririwa na Mwananchi.

“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini? alihoji Polepole huku akitaka kujua uwezo wa Nape kuikoa CCM.
“Ana nguvu kiasi gani kukibeba chama kikubwa Afrika? Wakati kiko shimoni yeye alikuwa wapi?
Akiendelea na mahojiano na Mwananchi, Polepole amemsihi Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Mangula ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ya Maadili ya CCM kumuwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
“Tuna kila sababu za kumshauri Mzee Mangula wa Kamati ya maadili kuwa hatuwezi kuwa na viongozi wa aina hii. Chama chenye watu milioni nane unakitoa shimoni na nini? Unakitoa na ngazi, ulitumia kamba kukitupia shimoni, uliita zimamoto?  Alihoji.
Wakati huo huo, Polepole amesema kuwa CCM kina mpango wa kujenga chuo kikuu kitakachotumika kuwafundisha makada wake kuhusu utaratibu, utamaduni na nidhamu ya chama.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post