RAHCO WAMJIBU ASKOFU GWAJIMA BAADA YA KUTANGAZA KUNUNUA TRENI BINAFSI

Kampuni Hodi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anaweza kuendesha huduma ya usafiri wa treni nchini Tanzania huku wakiwataka wawekezaji wengine wenye nia kama yake kujitokeza.
Hayo yalisemwa na Msemaji wa RAHCO, Catherine Moshi ambapo alieleza kuwa, kampuni hiyo imebariki uamuzi wa Askofu Gwajima wa kuwekeza kwa kununua treni, lakini wakamshauri, kabla ya kufanya hivyo ahakikishe amepata kibali kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Baraka hizo za RAHCO zimekuja ikiwa ni siku moja tangu Askofu Gwajima alipotangaza kanisani kwake kwamba ana mpango wa kununua treni itakayokuwa inawapeleka waumini kanisani lakini pia itabeba na abiria wa kawaida.
Akiendelea kufafanua jinsi Askofu Gwajima anavyoweza kutumia reli kuendeshea treni yake, Catherine alisema, atatakiwa kutoa taarifa RAHCO ili apewe njia kwa sababu mtumiaji wa reli ni Shirika la Reli Tanzania (TRL) pekee na atatakiwa kuelezea mabehewa atakayotumia ili apangiwe gharama husika.
Aidha, alisema hakuna sheria inayomzuia mtu kuwekeza katika miundombinu ya reli kwani kwenye baadhi ya nchi wanafanya hivyo na husaidia kukuza uchumi na kuimarisha sekta ya usafiri.
Catherine alisema watu wengi hawajawekeza kwenye miundombinu ya reli kwa sababu gharama zake ni kubwa sana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post