RAIS DKT MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa,  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenister Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
Sherehe za Muungano mwaka huu, zitafanyika katika Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika katika makao makuu ya nchi Mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma. April 24,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Pembeni yake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post