RAIS MAGUFULI ASEMA WALIOVUNJIWA NYUMBA MAGOMENI KOTA WATAKAA BURE MIAKA 5

Mhe. Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuwajengea nyumba wakazi wa Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam ambapo leo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 644 za wakazi hao waliovunjiwa nyumba zao na kubaki bila makazi.
Mhe. Rais Magufuli alitoa ahadi ya kuwajengea nyumba wakazi hao tarehe 09 Septemba, 2016 na ujenzi ukaanza tarehe 01 Oktoba, 2016 ambapo TBA inaendelea na kazi ya kujenga majengo matano yenye ghorofa 8 na 9 na yatakayokuwa na jumla ya nyumba 652, majengo ya biashara na bustani vitakavyokamilika mwaka huu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 20.
Mhe. Dkt. Magufuli amepongeza maendeleo ya ujenzi huo na baada ya kuelezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwa kuna maeneo mbalimbali nchini yenye nyumba zaidi ya 5,000 zilizo katika maeneo kama Magomeni Kota, ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya kuwapatia makazi bora wananchi kwa kuwajengea nyumba katika maeneo hayo.
“Nyumba hizi zikikamilika wapatieni hawa wakazi wa Magomeni Kota waliovunjiwa nyumba wakae bure kwa miaka mitano na baada ya hapo ndipo muwauzie kwa utaratibu mtakaouweka, lakini Mhe. Lukuvi najua nchi nzima kuna maeneo yana nyumba kama hizi za Magomeni kota 5,331 nilishaagiza nyumba hizo zirudishwe Serikalini na wewe mwenyewe umeahidi kuwa utaleta hati zake mwezi ujao, siku zote tulikuwa tunajenga nyumba kwa ajili ya wafanyakazi, sasa tutaanza kujenga nyumba kwa ajili ya watanzania, uwe mfanyakazi, uwe muuza chipsi uwe nani una haki ya kupata nyumba” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi waliokuwa wakiishi magomeni kota  kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam April 15,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi  wakishangilia  baada ya kukata utepe kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakati  akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Profesa Makame Mbarawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa kwa furaha na wasanii mbalimbali  wa filamu na wananchi wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Aprili, 2017
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post