RAYVANNY NA FAHYMA WAPATA MTOTO WA KWANZA. USOME UJUMBE ALIOANDIKA DIAMOND KWAO

Mwanamuziki Raymond maarufu Rayvanny kutoka kundi la WCB amefanikiwa kuvuka hatua katika maisha yake na sasa ni rasmi ataitwa Baba Jay.
Mwanamuziki huyo pamoja na mpenzi wake, Fahyma amejaliwa baraka ya kupata mtoto wao wa kwanza.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny alishindwa kujizuia na kuonyesha furaha yake ya kuitwa baba, huku akimpongeza mpenzi wake huyo kwa kupuuza ushauri wa baadhi ya watu waliomtaka atoe mimba hiyo, kwani kama angezaa angekuwa amjiharibia mipango ya maisha yake.
“Kuna Kuachana, kugombana,kutengana lakini kuacha yote hayo Swala Kubwa Sana Ulilolifanya Ambalo sitoweza kulisahau ni Kunipa @jaydanvanny kwenye maisha yangu.Maana Ungweza Kutoa Mimba lakini Ulikua Na nia njema na mwanao .Wengi walikushauri Utoe wakasema unajiharibia Future wakasema bado mapema lakini haukua tayari kumpoteza Mwanao. @fahyma_ @jaydanvanny We love you son #Youngparents๐Ÿ˜‚

Mama mtoto naye alimsifa Rayvanny na kusema kuwa katika maisha yake hajamuona kama yeye, Kiukweli kabisa bado sijamwona wa kufanana na wewe nakupenda sana baby @rayvanny na mwanangu kipenzi @jaydanvanny na mwomba mungu atuvushe salama๐Ÿ™
Lakini pia bosi wake, Mwanamuziki Diamond Platnumz alimpongeza Rayvanny kwa kujiunga na chama cha wababa ambapo amewaombea kwa Mungu awasaidie wamkuze nyema mtoto wao.
Congrats @rayvanny & @Fahyma_ on your first Born!… Inshaallah, Mwenyez Mungu awape Baraka, awalindie na wajalie kila lenye kheri ili Mumkuze vyema @jaydanvanny ….๐Ÿ™
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post