REAL MADRID WAONGOZA LIGI YA LA LIGA KWA TOFAUTI YA POINTI MBILI

Real Madrid wanaongoza ligi ya La Liga kwa tofauti ya pointi mbili, huku ikiwa imebakia michezo 10 baada ya kuifunga Alaves kwa magoli 3-0.

Karim Benzema alikifanya kikosi cha Zinedine Zidane kipate goli la kwanza baada ya kuunganisha pasi ya Dani Carvajal.

Deyverson na Edgar walipoteza nafasi za kuisawazisha goli Alaves kabla ya kufungwa tena magoli mawili katika dakika tatu.

Isco alifanya matokeo kuwa 2-0 kabla ya Nacho kuifungia Real Madrid goli la tatu kwa mpira wa kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Gareth Bale.
                       Mfaransa Karim Benzema akiachia shuti na kufunga goli la kwanza

                                    Mchezaji Isco akishangilia baada ya kutumbukiza goli la pili
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post