ROGER FEDERER AMFUATA RAFAEL NADAL FAINALI MICHUANO YA MIAMI OPEN

Roger Federer ameshinda mchezo mkali uliodumu kwa muda wa saa tatu dhidi ya Nick Kyrgios na kupata nafasi ya kutinga fainali dhidi ya Rafael Nadal katika michuano ya tenesi ya Wazi ya Miami.

Mchezaji huyo raia wa Uswizi ameshinda mchezo huo kwa seti 7-6 (11-9) 6-7 (9-11) 7-6 (7-5) na kufanya rekodi yake ya mwaka 2017 kufikia ushindi wa michezo 18 bila ya kupoteza hata mmoja.

Federer atamvaa Nadal kwa mara ya 37 siku ya jumapili, na mara ya pili kwa mwaka huu baada ya kumfunga Mhispania huyo mwezi Januari katika michuano ya tenesi ya Wazi ya Australia.
                    Roger Federer akipeana mkono na Nick Kyrgios baada ya kumshinda
                 Roger Federer akishangilia kwa kuiangalia kamera baada ya kushinda 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post