ROMA MKATOLIKI AMEWADANGANYA WATANZANIA KUHUSU KUTEKWA?

Kwa siku nne zilizopita, kumekuwapo na mjadala mzito sana kwenye mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na hata kwenye vijiwe vya kahawa kuhusu matukio ya utekaji wa watu yanayoendelea nchini. Wengi wa waliokuwa wakichangia mada hii walitamani sana kujua ni nani anayehusika na utekaji huu, na lipi hasa ni lengo lake.
Kilichochochea mjadala hii mzito, ni kutekwa kwa mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu waliokuwa katika studio za Tongwe Records usiku zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Tukio hili si la kwanza kutokea Tanzania, kwani yamewahi kutokea matukio mengine kama haya ikiwemo la Dkt Ulimboka, msaidizi wa Freeman Mbowe ambaye hadi leo hajulikani alipo, Ben Saanane. Marudio ya matukio haya niyo yaliyosababisha watu kuibua mjadala mzito kuhusu mhusika wa vitendo hivi vya utekaji.
Vyombo vya ulinzi navyo havikuwa nyuma kuhakikisha kuwa Roma na wenzake wanapatikana ili waweze kuungana na familia zao zilikuwa zimekumbwa na sintofahamu kuhusu hatma ya ndugu zao. Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema wanaendesha upelelezi kuhakikisha wasanii hao wanapatikana, kwani awali jeshi la polisi lilikanusha kuwashikilia wasanii hao.
Roma na wenzake walipatikana siku ya Jumamosi ikiwa ni muda mfupi baada ya Kamishna Sirro kuzungumza. Lakini awali Mkuu wa Mkoa alisema wasanii hao wangepatikana kabla ya Jumapili, jambo lililozua maswali kuhusu uhakika alioutoa kiongozi huyo kana kwamba anafahamu watu hawa walipo.
Upatikanaji wa Roma na wenzake uliwashtua wengi kwani taarifa zilizosambaa zilisema kuwa wapo Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam lakini hazikueleza walifikaje pale. Polisi hawakusema kama wasanii hao waliletwa na msamaria mwema, mwaliokotwa au walikuwa ndani ya kituo hicho, jambo lililoacha maswali mengi.
Sasa, licha ya kuwa wengi walifurahia kupatikana kwa wasanii hao, lakini furaha zile zimeanza kupotea baada ya tetesi kusambaa kwamba huenda tukio lile lilikuwa la kutengeneza na hata waliotekwa walikuwa wanalifahamu.
Tetesi hizo zinaonekana kuwakwanza wengi waliopigana kuhakikisha ndugu, jamaa au rafiki zao wanapatikana salama, lakini kumbe kwao ulikuwa ni mchezo. Wengine wamesema kuwa hata ambacho Roma alisema atawaambia Watanzania leo, hakina maana sababu ni sehemu ya mchezo wenyewe, na kuwa amepangiwa cha kuja kuzungumza.
Watu mbalimbali wameonyesha kusikitishwa kwao na tukio hili, licha ya kuwa hawakuandika moja kwa moja, lakini ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa, wanazungumzia tukio hili.
Hapa chini ni baadhi tu ya mengi yaliyoandikwa mitandaoni;


NI KWELI?
INASEMEKANA ISHU YA @Roma_Mkatoliki ALIPEWA DILI NA @paulmakonda ILI WATUYUMBISHE.
Roma amepatikana akiwa ameumia na yupo chini ya ulinzi,kuna maswali mengi sana kutoka kwa Polisi,Roma,na waliotangaza atapatikana kabla J2
WhatsApp Image 2017-04-10 at 10.49.59 AM

Haya yote yanayoendelea katika tukio hili yanaacha maswali mengi kwa mwananchi wa kawaida kuamini kipi hasa ni sahihi. Ni imani ya wananchi kuwa vyomboo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wahusika hao vitatoa majibu ya uhakika ambayo yatamaliza sintofahamu na mkanganyiko mkubwa uliopo ndani ya jamii kwa sasa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post