SABABU NYINGINE ZA KUFUKUZWA MKURUGENZI WA UNDP TANZANIA ZAIBULIWA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametoa taarifa iliyoeleza kuwa kuliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP), kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Awa Dabo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali ilifikia uamuzi huo kutokana na Bi. Dabo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya watumishi wenzake pamoja na menejimenti ya shirika hilo, hivyo kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.
Sakati hilo la kuondolewa kwa kiongozi hiyo limejadiliwa pia bungeni leo ambapo, Mbunge wa Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Pascal Yohana Haonga ameitaka serikali kueleza sababu halisi ya kiongozi huyo kuondolewa nchini.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, sababu iliyotolewa na serikali haitoshelezi kumpa mtu notisi ya saa 24 awe ameondoka nchini kisa tu hana uelewano mzuri na wafanyakazi wenzake.
Lakini pia mbunge huyo amesema kuwa uamuzi huo wa serikali unaichafua Tanzania katika medani ya kidiplomasia.
Gazeti la Mtanzania la leo Aprili 25 liliripoti taarifa ya kuondolewa nchini kwa Awa Dabo ambaye ni raia wa Gambia na kueleza kwamba aliondolewa wiki iliyopita akiwa chini ya ulinzi mkali.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, bosi huyo wa UNDP aliondolewa nchini baada ya kuingilia baadhi ya mambo katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015 pamoja na ule wa Machi 20, 2016.
“Kuondolewa kwa mkurugenzi huyo kumechangiwa pia na alichoandika katika ripoti yake kwenye Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu utata wa uchaguzi wa Zanzibar. 
Lakini pia jambo jingine lililosababsisha ni kuwasikiliza baadhi ya viongozi walioshindwa kwenye uchaguzi huo na kuwapa mbinu za kuwasilisha malalamiko kwa vyombo vya kimataifa.
“Je! Hata kama ingekuwa wewe unaingiliwa mambo yako ya ndani na mtu ambaye si raia wa nchi yako, unaweza kuvumilia? jibu jepesi hapana.” liliandika gazeti hilo.
Hapa chini ni maoni ya baadhi ya watumiaji wa mitandao kuhusu tukio hilo;
Tanzania UNDP director AwaDabo expelled her over "strained relations" w/staff. Many think its harsh criticism of 2016 polls in Zanzibar-BBC
Expelling  Country Director Awa Dabo is not a solution to the  electoral crisis.  must be held accountable for this.
Bosi UNDP "haelewani na watumishi wenzie (wa UNDP)," serikali yamtimua within 24 hrs yet Daudi Bashite na midhambi yote aliyonayo HAGUSWI!

Watu wengi wanaona kuondolewa kwa bosi huyo kuwa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko zile za kiutendaji zilizoelezwa katika taarifa ya serikali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post