SAKATA LA POINTI 3 KATI YA KAGERA SUGAR NA SIMBA LAFIKIA MWISHO

Baada ya takribani wiki moja ya mvutano mkali na mjadala usiokuwa na mwisho wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), sakata la alama tatu linalozihusisha klabu za Simba na Kagera Sugar linatarajiwa kufikia tamati leo ambapo kamati hiyo itakapotoa uamuzi wa mwisho.
Sakati hili lilikuwa kubwa zaidi baada ya Simba kupewa alama tatu na Kamati ya Saa 72 kufuatia madai kuwa Kagera Sugar walimchezesha Mohammed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano, jambo ambalo ni kosa.
Kufuatia maamuzi hayo, Kagera Sugar ilikwenda katika Kamati ya Katiba kukata rufaa kupinga maamuzi ya Kamati ya Saa 72 wakidai kuwa Fakhi hakuwa na kadi tatu za njano kama ilivyodaiwa, bali alikuwa na kadi mbili na hivyo warejeshewe alama zao tatu na magoli.
Kwa muda wote wa takribani wiki moja kamati haikuweza kutoa uamuzi, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Richard Sinamtwa amesema kuwa wajumbe wote watakutana leo na mashahidi wote na watafikia hitimisho na kuamua timu ipi ilistahili alama tatu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post