SAKATA LA VYETI VYA BASHITE LAMPONZA ASKOFU WA KKKT IRINGA

Sakata la vyeti vya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda limezidi kuchukua sura mpya nchini ambapo sasa limefika mbali na kuzidi kuwahusisha viongozi wengine wa dini.
Kiongozi ambaye zamu hii amezungumzia sakata hilo la vyeti ni Askofu  Mstaafu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa, Dkt. Owdenburg Mdegella ambapo amewataka wananchi kujikita katika shughuli za  kiuchumi badala ya kupoteza muda  mwingi  kujadili  mambo  ya  vyeti vya Daud Bashite.
Askofu Mdegella aliyasema hayo wakati  akitoa  salamu  za Pasaka katika  usharika  wa kanisa kuu, ambapo alidai kuwa watanzania wanapoteza  muda  mwingi kwa jambo hilo badala ya  kushughulika na mambo ya msingi yenye  tija kwa  Taifa.
Image result for Owdenburg MdegellaAskofu  Mstaafu wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa, Dkt. Owdenburg Mdegella
Kauli ya Askofu huyo imeshambuliwa vikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wamemtaka kutowapangia nini cha kufanya badala yake ajikite na shughuli za kanisa.
Hapa chini ni baadhi ya maoni ya watu waliyotoa kuhusu kauli ya Askofu Mdegella. Unaweza kusoma maoni zaidi kwa kubonyeza hapa.
34
Kauli ya Askofu huyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Rais Dkt Magufuli aliposema kuwa anasubiri ripoti ya watumishi wa serikali wenye vyeti feki ili aweze kuifanyia kazi.
Rais Dkt Magufuli aliyasema hayo wakati akizindua mabweni maywa ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo alisema watumishi wa serikali wanaokadiriwa kufiki 9,000 wanavyeti feki.
Kwa muda sasa kumekuwapo na tuhuma kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitumia vyeti vya mtu mwingine baada ya kufeli kidato cha nne. Inadaiwa kuwa jina analotumia sasa, Paul Makonda si la kwake ni la mwenye vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite.
Licha ya tuhuma hizi kuzungumzwa kila mara, kiongozi huyo hakuwahi kusema kama ni kweli au la.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post