SIMU INAVYOCHANGIA KUPUNGUZA UFANISI KAZINI

SHARE:

Na Jumia Travel Tanzania Inawezekana wewe ni miongoni wa watu wasioweza kustahimili kukaa mbali na simu hata kwa dakika moja. Ni suala ...

Na Jumia Travel Tanzania
Inawezekana wewe ni miongoni wa watu wasioweza kustahimili kukaa mbali na simu hata kwa dakika moja. Ni suala gumu sana kwa wengi wetu kuweza kuitelekeza simu na kufanya shughuli nyingine kama vile tukiwa ofisini. Lakini je ushawahi kujiuliza kuna madhara gani kwa kuiendekeza tabia hiyo?
Kutokana na kukua kwa teknolojia simu imekuwa ni kifaa muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya binadamu kwani kinamfanya kuwa anapatikana kwa urahisi muda wowote. Jumia Travel imeelezea kwa kifupi katika makala haya athari na namna ya kudhbiti matumizi ya simu ukiwa mahala pako pa kazi.
Kwanza kabisa simu hupoteza muda mwingi kama usipopangilia ni wakati gani wa kuwa nayo na wakati gani sio. Suala hili liko wazi kwa sasa hususani uwepo wa programu nyingi zinazozidi kuvumbuliwa kila kukicha kama vile facebook, twitter, whatsapp, linkedin, pinterest, snapchat, nakadhalika.
Programu hizi humhitaji mtu kuzitumia muda wote kutokana na ushirikishwaji wa taarifa kutoka marafiki na vyanzo mbalimbali vya habari. Kupotea kwa muda kutakuja kama na wewe utataka kufuatilia kila jambo linaloendelea kwenye mitandao hii.
Usipokuwa muangalifu pia utapoteza umakini kwenye shughuli zako unazozifanya. Hii inaweza kutokea wakati upo katikati ya kazi fulani na ghafla ukapigiwa simu au ukapokea ujumbe au ishara fulani kutoka kwenye programu zilizopo kwenye simu yako.
Sio watu wote wanaoweza kujizuia kutojibu simu au jumbe au pengine kupitisha macho kwenye aidha ya programu hizo. Zipo tafiti nyingi tu zinazoelezea ni namna gani umakini hupotea kutokana na ishara zinazotokana na simu.
Kutomaliza kazi kwa wakati. Hii inaweza kusababishwa na kila mara kutumia muda kutaka kujibu au kujua kila kitu kinachoendelea kwenye simu yako. Kwa mfano, kama umejiunga kwenye makundi kadhaa ya mtandao wa Whatsapp na mlikuwa mnajadili kuhusu tukio la kusisimua linaloendelea kwa wakati huo; sidhani kama utaweza kutotazama simu yako pindi ujumbe ukiingia huku ukiwa katikati ya kazi fulani.
Sidhani kama watu wengi wameshagundua kwamba hili ni tatizo. Wafanyakazi wengi wanachokifanya ni kujificha tu ili wasionekane na mabosi wao lakini si kujizuia wasitumie kabisa simu zao.
Unawezaje basi kuiepuka hali hii ambayo inawatesa watu wengi? Zifuatazo ni mbinu chache endapo ukizizingatia unaweza kufanikiwa kuwa na udhibiti juu ya simu yako.
Zima sauti ya simu yako. Ni vema ukazima sauti ya simu yako (mute) kama una kazi nyingi na tena zinazohitaji umakini wako wa hali juu. Hii itakusaidia kuwa na utulivu bila ya muingiliano wa simu, ujumbe mfupi au milio ya sauti za programu zilizomo kwenye simu. Unaweza kufanya kwenye kipindi maalumu ili pia uwe na fursa ya kufanya mawasiliano mengine muhimu na watu wanaokuzunguka.
Weka mbali simu yako. Kama unaona hauwezi kupitisha hata dakika 10 bila ya kuigusa simu yako, inashauriwa pia ukaiweka mbali. Kwa mfano unaweza kuiweka kwenye droo mahali unapokaa au ukampatia mfanyakazi wako akakuhifadhia na kisha kukurudishia pindi utakapomaliza kazi zako. Hii itakufanikishia kumaliza kazi ulizonazo kwa umakini, ufanisi na wakati bila ya bugudha yoyote ile.
Pangilia muda wa kuwa na simu yako. Pia inashauriwa kupangilia muda maalumu wa kuwa na simu yako ili kujua masuala mbalimbali yaliyotokea wakati uko mbali nayo. Kwa mfano, unaweza pengine ukatenga kila baada ya saa moja au mawili ndiyo unashika simu yako au hata wakati wa kupata chakula cha mchana.
Kama hauna shughuli yoyote ambayo itahitaji simu yako kuwa mkononi muda wote basi mbinu hii ni bora zaidi. Kwanza itakupatia muda wa kutosha kuweza kuperuzi na kujibu jumbe na taarifa mbalimbali kwa pamoja huku ukiwa huna wasiwasi wa kushikwa na bosi wako.
Wafahamishe watu unaowasiliana nao mara kwa mara kwamba utakuwa mbali na simu yako. Endapo utakuwa mbali na simu yako au itakuwa katika hali ya kutotoa sauti au ishara yoyote ile basi ni vizuri ukawafahamisha watu unaowasiliana nao mara kwa mara ili wasikutafute. Hii pia inaweza kusaidia hata kupungua kwa kupokea simu na jumbe nyingi wakati wa kazi.
Kila mabadiliko huja na faida na hasara zake hivyo hatuna budi kujifunza kuendana nayo. Mabosi wengi kwa sasa wanawalalamikia wafanyakazi wao kutumia muda mwingi kwenye simu zao, hasa mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi. Kupitia mbinu hizi kadhaa zilizotolewa na Jumia Travel, tunaamini kwamba kuanzia sasa utaanza kudhibiti matumizi ya simu yako ili kulinda kibarua chako kisiote nyasi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SIMU INAVYOCHANGIA KUPUNGUZA UFANISI KAZINI
SIMU INAVYOCHANGIA KUPUNGUZA UFANISI KAZINI
https://4.bp.blogspot.com/-XGNB2pvrdUo/WOD3j-AceVI/AAAAAAAAZBQ/im860ZLBnYYn1oTgpzEwLkRMyl05Sl_zwCLcB/s1600/1-750x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-XGNB2pvrdUo/WOD3j-AceVI/AAAAAAAAZBQ/im860ZLBnYYn1oTgpzEwLkRMyl05Sl_zwCLcB/s72-c/1-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/simu-inavyochangia-kupunguza-ufanisi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/simu-inavyochangia-kupunguza-ufanisi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy