SIMU YAMPONZA BINTI ALIYEJIRUSHA BAHARINI

SHARE:

Msichana mmoja (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa mika 16 na mwanafunzi wa kidato cha 3 huko Zanzibar, juzi alijitosa baharini katika en...

Msichana mmoja (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa mika 16 na mwanafunzi wa kidato cha 3 huko Zanzibar, juzi alijitosa baharini katika eneo la Chumbe kutoka katika boti ya Azam Marine Kilimanjaro V.
Msichana huyo aliyekuwa akisafiri na mjomba wake kutoka Dar es salaam kwenda Unguja alijirusha baharini majira ya saa 5 na kuokolewa na mabaharia wa boti hiyo ndani ya muda mchache.
Wanafamilia wa binti huyo waishio eneo la Kikwajuni Unguja walieleza kuwa kabla ya kutoroka kwa binti huyo, walimkuta na simu ambayo hawakufahamu alikoipata. Kutokana na utaratibu wa familia hiyo ya kutoruhusu simu kwa watoto, walimnyang’anya simu hiyo na kumtaka aeleze alikoitoa vinginevyo watampeleka Polisi. Binti huyo alikasirishwa na kitendo hicho ndipo alipofanya uamuzi wa kutoroka.
Mama mdogo wa binti huyo alieleza kuwa walimtafuta binti huyo bila mafanikio ndipo walipoamua kuipekua simu aliyokuwa akiitumia na kukuta namba ya kijana mmoja iliyokuwa imetumiwa mara nyingi. Walipowasiliana na kijana huyo kumuuliza anafahamiana vipi na yule binti, alijibu kuwa walijuana kupitia mtandao wa ‘facebook’ lakini hawajawahi kukutana kwa kuwa binti anaishi Zanzibar na kijana anaishi Dar es Salaam.
Alisema walimpa taarifa kijana huuyo kuwa binti yao ametoroka na hajulikani alikokwenda, hivyo kumwomba kusaidiana kuhakikisha wanampata akiwa salama.
“Kwa kweli kijana huyo alikubali kutoa ushirikiano na akawa anawasiliana na binti yetu na kumuleza kuwa yuko Dar es Salaam na amehifadhiwa na dereva teksi baada ya kukosa msaada wa eneo analotaka kwenda ambako ni kwa bibi yake anayeishi Mburahati, Dar es Salaam” alisema
Alisema aliwasiliana na dereva huyo aliyemuhifadhi binti yao na kuambiwa kwamba amesharipoti katika serikali ya mtaa anoishi kuwa amemuokota binti huyo bandarini , Dar es salaam baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata msaada.
Mama mdogo ambaye ndiye aliyemlea binti huyo tangu akiwa mdogo alieleza kwamba mama mzazi wa  binti huyo anaishi Muscat, Oman, na alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kupata taarifa kuwa binti yake amejitupa baharini wakati akitokea Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa siku kadhaa na hatimaye kupatikana.
Naye mjomba wa binti huyo ambaye ndiye aliyekwenda Dar es Salaam kumchukua, alieleza kuwa wakiwa ndani ya boti binti alilalamika kuwa anajisikia vibaya, hivyo anahitaji kwenda kukaa kwenye veranda ya boti ili apunge upepo. Wakatoka kwenda kwenye veranda nje ya boti hiyo.
Wakiwa wamekaa binti huyo alimtaka mjomba wake kumpatia kitambaa cha kufunika uso ‘nikabu’ na baibui avae ili kuepuka usumbufu wakati wa kushuka kwani muda wa kufika Zanzibar ulikuwa umekaribia.
Mjomba alipogeuka upande wa pili ili kuvichukua vitu hivyo  katika begi, ndipo ghafla msichana huyo alijitosa ndani ya bahari.
“Nilipiga yowe baada ya kuangalia na kumwona. Tulishirikiana na mabaharia wa boti hiyo  ili kumwokoa na ndani ya muda mchahe tulifanikiwa”  alisema
Wanafamilia wa binti huyo walisema binti huyo alikuwa na tabia nzuri tokea alipokuwa mdogo, na mara nyingi alipendelea kukaa ndani. “Hatujui kwa nini amliamua kufanya uamuzi huo”
Aidha daktari Suleiman Abdul, Mratibu wa huduma za afya Hospitali ya Kidongo Chekundu alikotibiwa msichana huyo, alisema wanaendelea na uchunguzi wa afya ya akili ya msichana huyo na kuwataka wanafamilia yake kutokuzungumzia chochote kuhusu tukio hilo na waendelee kushirikiana nae vizuri ili kuona maendeleo ya afya yake.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SIMU YAMPONZA BINTI ALIYEJIRUSHA BAHARINI
SIMU YAMPONZA BINTI ALIYEJIRUSHA BAHARINI
https://2.bp.blogspot.com/-OLi4NbiMVoI/WOTK80Yh9sI/AAAAAAAAZHU/1ZyCireh_fEnGD-ax11efHful8icwdSGACLcB/s1600/x45292-750x375.jpg.pagespeed.ic.ufqWlXNnIM.webp
https://2.bp.blogspot.com/-OLi4NbiMVoI/WOTK80Yh9sI/AAAAAAAAZHU/1ZyCireh_fEnGD-ax11efHful8icwdSGACLcB/s72-c/x45292-750x375.jpg.pagespeed.ic.ufqWlXNnIM.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/simu-yamponza-binti-aliyejirusha.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/simu-yamponza-binti-aliyejirusha.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy